KARISMATIKI KATOLIKI: Sehemu ya I: Neno Karismatiki linatokana na maneno ya Kiyunani “Karis” na “Charisma neno charis lina maana ya upendeleo, majaliwa au neema. Neno charisma ambalo uwingi wake ni charismata, linamaanisha zawadi maalum ya kiroho anayojaliwa mtu (Mkristo) kwa neema ya Mungu. Kwa maneno mengine charisma ni zawadi ya kiroho katika maana maalum, kwa misingi ya maana hizi mwanadamu hawezi kuzitawala karama katika upatikanaji wake, isipokuwa zinatolewa na Roho Mtakatifu kwa kadiri ya hiyari na mahitaji ya huduma katika mwili wa Kristo, yaani Kanisa (rej 1Kor 12:8) Kumbe neno “Karismatiki” linapotumika kama nomino, linamwakilisha mtu aliyepata na anayetumia karama za kiroho za Roho Mtakatifu. Kimsingi kila Mkristo mbatizwa kwa mujibu wa Ubatizo na Kipaimara ni Mkarismatiki, kwani amempokea Roho aliye mtoaji wa karama (1Kor 12:28-30) naye anapaswa kuzitumia karama zake kwa huduma ya Kanisa lote. KARISMATIKI KATOLIKI NI NINI Karismatiki Katoliki siyo Chama cha Kitume, ba...
Comments
Post a Comment