IFAHAMU KARISMATIKI KATOLIKI
- Get link
- X
- Other Apps
KARISMATIKI KATOLIKI:
Sehemu ya I:
Neno Karismatiki linatokana na maneno ya Kiyunani “Karis” na “Charisma neno charis lina maana ya upendeleo, majaliwa au neema. Neno charisma ambalo uwingi wake ni charismata, linamaanisha zawadi maalum ya kiroho anayojaliwa mtu (Mkristo) kwa neema ya Mungu. Kwa maneno mengine charisma ni zawadi ya kiroho katika maana maalum, kwa misingi ya maana hizi mwanadamu hawezi kuzitawala karama katika upatikanaji wake, isipokuwa zinatolewa na Roho Mtakatifu kwa kadiri ya hiyari na mahitaji ya huduma katika mwili wa Kristo, yaani Kanisa (rej 1Kor 12:8)
Kumbe neno “Karismatiki” linapotumika kama nomino, linamwakilisha mtu aliyepata na anayetumia karama za kiroho za Roho Mtakatifu. Kimsingi kila Mkristo mbatizwa kwa mujibu wa Ubatizo na Kipaimara ni Mkarismatiki, kwani amempokea Roho aliye mtoaji wa karama (1Kor 12:28-30) naye anapaswa kuzitumia karama zake kwa huduma ya Kanisa lote.

KARISMATIKI KATOLIKI NI NINI
Karismatiki Katoliki siyo Chama cha Kitume, bali mkondo mmojawapo katika Kanisa na ni mwamko wa Kanisa zima kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Mwamko huu unawajumuisha wanakanisa wote walio na wasio kwenye vyama mbalimbali vya kitume, mkondo huu unavuviwa na Roho Mtakatifu ambaye ndiye aliyepewa jukumu la kumshuhudia Kristo, kwa kutakatifuza, kufundisha, kuongoza, kumkumbusha, kuwasaidia watu kutumia karama zao n.k. Lakini katika muktadha wa mikondo inayozaliwa na Kanisa, neno Karismatiki siku hizi linatumika kumaanisha upyaisho wa Roho Mtakatifu.
Kwa kunyoosha maneno, Karismatiki Katoliki ni kikundi cha Sala kinachotakiwa kustawisha karama za wanadamu na kuwasaidia kwazo wapate wokovu. Ni kikundi cha kusali kikiwasaidia wote kumakinika na karama zao za kiroho kwa utukufu wa Mungu, kukua kwa Kanisa na wokovu wa wanadamu wote.
Itaendelea…
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment