SEHEMU YA PILI.

 SEHEMU YA PILI.



MIZIZI YA KARISMATIKI KATOLIKI KATIKA KARNE YA 19.

Upyaisho wa Karismatiki wa siku ya leo una mizizi katika karne ya kumi na tisa. 

Kati ya mwaka 1895 na 1903 mwenyeheri Sr. Elena Guerra ambaye ni mwanzilishi wa shirika la masista wa Oblate wa Roho Mtakatifu huko Italia, aliandika barua takribani 12 kwa Papa Leo XIII ambapo alimuomba kuhimiza zaidi ibada kwa Roho Mtakatifu kati ya wakristo wakatoliki.


Katika kujibu maombi ya sista Elena, Papa Leo XIII aliandika barua ya kichungaji  ijulikanayo kama (Encyclical, Divinum Illud Munus 1897)


Katika barua hiyo baba mtakatifu alilisihi kanisa zima kusali novena kwa ajili ya pentekoste ili kuanza karne mpya.


Kuanzia hapa kwa Sr Elena ndipo mkondo wa Karismatiki katoliki hukita mizizi yake na kuonekana kwamba ulianza ndani ya wanakanisa wenyewe.


Mwanzo wa karne ya 20.

Karne ya ishirini iliangazwa zaidi na wimbi la upentekoste ambapo liliingia hadi kwenye jumuiya za makanisa ya Kiprotestanti.


Januari 1, 1901 papa Leo XIII alisali kwa Roho Mtakatifu na kuimba wimbo wa Uje Roho Muumbaji katika dirisha la Basilika la Mtakatifu Petro huko Roma.


Siku hiyo hiyo katika chuo na shule ya biblia iitwayo Betheli huko Kansas, Marekani, Roho Mtakatifu aliwashukia na kuwajaza baadhi ya wanakikundi wa kiprotestanti waliokua wakiomba kupokea Roho Mtakatifu kama mitume wa kanisa la kwanza walivyo mpokea.


Mmoja wa wanafunzi aitwaye Agness Ozman alianza kunena kwa lugha ambapo lilikua ni jambo jipya miongoni mwao na kwa wakati ule.

Baada ya tukio hilo vuguvugu la upentekoste lilianza kujikita zaidi katika makanisa ya kiprotestant na muinjilisti Charles Parham aliita kunena kwa lugha kuwa ni “ uthibitisho wa kibiblia wa kubatizwa na kujazwa Roho Mtakatifu” huyu muinjilisti ndiye aliyeanzisha na kuhimisha huu mkondo wa upentekoste katika karne ya 20. Baadaye walifuatia watu wengine kama vile William Seymour ambaye alipokea mafundisho ya Kipentekoste kutoka kwa Charles Parham yeye akiwa huko Hauston, Texas, Marekani.


Kati ya mwaka 1906-1909 kwa kupitia kile kilichoitwa Azusa Street Revival, upentekoste ulienea ulimwenguni kupitia uongozi wa William Seymour. 


Kati ya miaka hii ya 1906-1907 ilifanyika mikutano kadha wa kadha ya kipentekoste huko Oslo, kisha Scandnavia, Uingereza na Ujerumani. Makanisa kadhaa ya kiprotestanti yalianza kupokea mkondo huu wa Upentekoste ambao ulikazia swala la Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha. 


1909 Luigi Francescon na Giacomo Lombardi hawa walianzisha upentekoste katika nchi ya Italia, Argentina Brazili na baadhi ya Maeneo ya USA ambayo mkondo huu haukupenyeza mwanzoni. 


Machimbuko ya ndani kabisa ya mkondo huu wa kipentekoste yana mhusisha muinjilisti mkongwe wa uingereza John Wesley wa kanisa la kimethodisti huyu aliishi kati ya mwaka 1703- 1791.


John Wesley alijikita katika kueneza injili maeneo mbalimbali ya uingereza alianzisha mkondo uliojulikana kama “Holy Club” ambapo Wesley alikazia zaidi kuhusu utakatifu wa maisha ya kikristo. Wakati huu kundi hili halikuwa na muonekano wowote wa upentekoste ila unatajwa kuchangia mwamko wa upentekoste katika karne ya 20. John Wesley alijihusisha pia na kuhubiri injili maeneo tofauti tofauti huku akiwatuma na waandamizi wengine ambao walijulikana kama wainjilisti. Ikumbukwe kuwa yeye alikazia zaidi kuhusu utakatifu wa maisha na ukamilifu wa maisha ya kikristo yaani “Christian Perfection” hii ndo historia ya zamani zaidi ambapo baadaye inaunganishwa na upentekoste na Upyaisho wa Karismatiki katoliki.


Itaendelea

 

Kwa nini  Upyaisho wa Karismatiki Katoliki unahusishwa na madhehebu ya Kiprotestanti na upentekoste wa kilokole?

Comments

Popular posts from this blog

IFAHAMU KARISMATIKI KATOLIKI