Posts

Je unajua Karismatiki ilipoanzia?

  Charismata, in Greak, maana yake ni Zawadi, 1967 Dukwen University, 1993 ICCRS was instituted 1985 office za Karismaki zilianzishwa Malengo: NB Malengo ya Kanisa, ndiyo malengo ya Kanisa Katoliki Luk4:19-19 au Mathayo 28:18-20, Canon Law a210-2011. 1.Kusaidia watu wakue na kuendelea katika mahusiano binafsi na Utatu Mtakatifu: To Encounter with the person of Jesus Christ in your life. 2.Kuwasaidia watu wajue umuhimu wa Roho mtakatifu katika kuwaongoza, Kujue uwezo na kuonja nguvu za Roho mtakatifu 3.Kuwasaidia watu wapokee na kutumia karama za Roho mtakatifu latika kukijenga kanisa 4. Kufanya uinjilishaji kwa nguvu za Roho Mtakatifu. "Twendeni masokoni tuwahubirie, masokoni, mashambani, na kila mahali tuwahubirie watu wote habari njema" Rom10:17 Kuinjilisha walioko ndani ya kanisa, mifumo ya kijamii, 5. Kumshuhudia Yesu kwa maneno na kwa matendo. 6. Kusaidia watu kukua katika utakatifu, utume, ushiriki wa Sakramenti za kanisa, na kudumisha umoja wa kanisa kwa kuhimiza yale ...

KWANINI UPYAISHO WA KARISMATIKI KATOLIKI UNAUSISHWA NA MADHEHEBU MENGINE

Image
KWANINI  UPYAISHO WA KARISMATIKI KATOLIKI  UNAUSISHWA NA MADHEHEBU YA KIPROSTANTI NA UPETEKOSTE WA KILOKOLE  Kwa nini Upyaisho wa Karismatiki Katoliki unahusishwa na madhehebu ya Kiprotestanti na upentekoste wa kilokole.? Tunasoma katika Yoh 3:8 kwamba “Upepo huvuma upendako na sauti yake waijua lakini hujui unakotoka wala unakokwenda...” Baada ya John Wesley mwanzilishi wa makanisa ya kimethodist kufariki na ambaye pia anaonekana kuhimiza juu ya utakatifu wa maisha na kuhubiri injili kwa nguvu za Roho Mtakatifu miaka ya 1700s ubaridi na ukimya uliendelea hadi Sr Elena Guera alipopata msukumo wa kuhimiza tena juu ya Roho Mtakatifu ndani ya Kanisa Katoliki mwaka 1895. Baada ya barua za Sista huyu kujibiwa na Baba mtakatifu Leo XIII ndipo ilipotungwa sala ya “uje Roho Mtakatifu” na kuanza kusaliwa na waamini. Ukimya uliendelea kutawala ndani ya Kanisa na hapakuwa na mkazo tena Juu ya Roho Mtakatifu na namna ya kuishi maisha binafsi na kuhusiana na Mungu kwa namna ya kipekee...

SEHEMU YA PILI.

Image
 SEHEMU YA PILI. MIZIZI YA KARISMATIKI KATOLIKI KATIKA KARNE YA 19. Upyaisho wa Karismatiki wa siku ya leo una mizizi katika karne ya kumi na tisa.  Kati ya mwaka 1895 na 1903 mwenyeheri Sr. Elena Guerra ambaye ni mwanzilishi wa shirika la masista wa Oblate wa Roho Mtakatifu huko Italia, aliandika barua takribani 12 kwa Papa Leo XIII ambapo alimuomba kuhimiza zaidi ibada kwa Roho Mtakatifu kati ya wakristo wakatoliki. Katika kujibu maombi ya sista Elena, Papa Leo XIII aliandika barua ya kichungaji  ijulikanayo kama (Encyclical, Divinum Illud Munus 1897) Katika barua hiyo baba mtakatifu alilisihi kanisa zima kusali novena kwa ajili ya pentekoste ili kuanza karne mpya. Kuanzia hapa kwa Sr Elena ndipo mkondo wa Karismatiki katoliki hukita mizizi yake na kuonekana kwamba ulianza ndani ya wanakanisa wenyewe. Mwanzo wa karne ya 20. Karne ya ishirini iliangazwa zaidi na wimbi la upentekoste ambapo liliingia hadi kwenye jumuiya za makanisa ya Kiprotestanti. Januari 1, 1901 papa L...

IFAHAMU KARISMATIKI KATOLIKI

Image
  KARISMATIKI KATOLIKI: Sehemu ya I: Neno Karismatiki linatokana na maneno ya Kiyunani “Karis” na “Charisma neno charis lina maana ya upendeleo, majaliwa au neema. Neno charisma ambalo uwingi wake ni charismata, linamaanisha zawadi maalum ya kiroho anayojaliwa mtu (Mkristo) kwa neema ya Mungu. Kwa maneno mengine charisma ni zawadi ya kiroho katika maana maalum, kwa misingi ya maana hizi mwanadamu hawezi kuzitawala karama katika upatikanaji wake, isipokuwa zinatolewa na Roho Mtakatifu kwa kadiri ya hiyari na mahitaji ya huduma katika mwili wa Kristo, yaani Kanisa (rej 1Kor 12:8) Kumbe neno “Karismatiki” linapotumika kama nomino, linamwakilisha mtu aliyepata na anayetumia karama za kiroho za Roho Mtakatifu. Kimsingi kila Mkristo mbatizwa kwa mujibu wa Ubatizo na Kipaimara ni Mkarismatiki, kwani amempokea Roho aliye mtoaji wa karama (1Kor 12:28-30) naye anapaswa kuzitumia karama zake kwa huduma ya Kanisa lote. KARISMATIKI KATOLIKI NI NINI Karismatiki Katoliki siyo Chama cha Kitume, ba...