KWANINI UPYAISHO WA KARISMATIKI KATOLIKI UNAUSISHWA NA MADHEHEBU MENGINE

KWANINI  UPYAISHO WA KARISMATIKI KATOLIKI  UNAUSISHWA NA MADHEHEBU YA KIPROSTANTI NA UPETEKOSTE WA KILOKOLE


 Kwa nini Upyaisho wa Karismatiki Katoliki unahusishwa na madhehebu ya Kiprotestanti na upentekoste wa kilokole.?


Tunasoma katika Yoh 3:8 kwamba “Upepo huvuma upendako na sauti yake waijua lakini hujui unakotoka wala unakokwenda...”


Baada ya John Wesley mwanzilishi wa makanisa ya kimethodist kufariki na ambaye pia anaonekana kuhimiza juu ya utakatifu wa maisha na kuhubiri injili kwa nguvu za Roho Mtakatifu miaka ya 1700s ubaridi na ukimya uliendelea hadi Sr Elena Guera alipopata msukumo wa kuhimiza tena juu ya Roho Mtakatifu ndani ya Kanisa Katoliki mwaka 1895.


Baada ya barua za Sista huyu kujibiwa na Baba mtakatifu Leo XIII ndipo ilipotungwa sala ya “uje Roho Mtakatifu” na kuanza kusaliwa na waamini.


Ukimya uliendelea kutawala ndani ya Kanisa na hapakuwa na mkazo tena Juu ya Roho Mtakatifu na namna ya kuishi maisha binafsi na kuhusiana na Mungu kwa namna ya kipekee.


Wakati huo ikumbukwe kuwa mwaka 1901 ndipo vuguvugu la upentekoste lilianza rasmi na kuenea sehemu mbali mbali ulimwenguni likiongozwa na mwinjilisti Charles Parham.


Ni wazi kuwa ndani ya kanisa himizo la Roho Mtakatifu lilipoa baada ya Sr Elena na badala yake Upentekoste ukaanza kukolea katika madhehebu mengine.


Kimsingi hii ndio sababu kubwa wengi huiona Karismatiki kuwa na mizizi ya kipentekoste kwani jambo ambalo lilianza kuonekana kwetu halikupewa mkazo sana badala yake wengine walifunuliwa kwa namna yao na kulifanyia kazi na baadaye likarudi tena ndani ya Kanisa katoliki.


Maandalizi ya Mtaguso wa Pili wa Vatikano

Katika kuandaa mtaguso huu ndipo tena baada ya miaka mingi kupita Baba Mtakatifu Yohane XXIII mwaka 1962 alisali tena akimwomba Mungu kupyaisha maisha ya wanakanisa kama katika Pentekoste ya kwanza. 


Wikiendi ya Duquesne

Baada ya kumalizika kwa mtaguso wa pili wa vatikano 1965 ambapo pia kulikua na himizo juu ya kuhusiana binafsi na Mungu kwa namna ya kipekee na Roho Mtakatifu. 


mwaka 1967- Tukio linalohesabiwa na wengi kuwa ni mwanzo wa Upyaisho Karismatiki Katoliki, ni tukio

linaloitwa kwa kiingereza ‘Duquesne Weekend’ (Mwisho wa Juma wa Dukeni). Hakika yako

matukio mengine ya mlipuko huu yaliyotokea wakati huo huo lakini tukio la Dukeni ndilo

lililoandikwa zaidi kuliko mengine.

Tukio la mwisho wa juma la Dukeni lilitokea hivi, 

Kikundi cha wakufunzi walei wa Chuo Kikuu cha Dukeni kinachoendeshwa na Mapadre wa

Shirika la Roho Mtakatifu (Duquesne University of the Holy Spirit), huko Pittsburgh, Marekani,

walianza kukutana kwa miezi kadhaa wakijaribu kutafakari kile kinachopungua katika maisha yao

binafsi. Hatimaye hawa hatimaye hawa walivutiwa kuhudhuria mkutano wa sala wa Upyaisho

Karismatiki(waprotestant) uliokuwa ukiendeshwa na Waepiskopali katika eneo lao kama namna ya kujifunza.

Wawili kati yao walirudi kwenye mkutano huo juma moja baadaye na wakabatizwa katika Roho

Mtakatifu. Hawa wawili walikuwa mwanzo wa Ubatizo wa Roho mtakatifu kuwafikia

watu kadhaa hapo chuoni. Hatimaye wale waliopokea ubatizo wa Roho Mt. waliwaalika wengine wachache,

wengi wao wakiwa vijana wanafunzi katika mafungo ya mwisho wa juma (Februari 17-18,1967)

kwa lengo la kuwaombea Ubatizo katika Roho Mtakatifu. Hili ndilo tukio maarufu la mwisho wa

juma wa Dukeni.


Wale vijana wote wakabatizwa katika Roho Mtakatifu. Mmoja wao ni Patricia Galagher

Mansfield ambaye ambaye ameueleza ushuhuda wake mahali pengi. Mwezi mmoja

baadaye Machi, 1967, Ralph Martin, Steve Clark, Gerry Rauch na Jim Carvanar ambao walikuwa

viongozi wa kitaifa wa Kursilo(vugu vugu la kiroho), walitembelea Dukeni. Huko walikuta moto

umeanza na wao pia wakabatizwa katika Roho Mtakatifu. Baadaye hawa wane walirejea vituoni

kwao kwenye vyuo vikuu vya Michigan na Notre Dame ambako walisambaza mota na hivyo

Upyaisho Karismatiki Katoliki(UKK) ukaanza kuenea. UKK ulienea kwa kasi sana Marekani kote na

nje ya Marekani. Miaka minane baadaye Ralph Martin mmoja wa viongozi wa mwanzo kabisa

wa Upyaisho Karismatiki Katoliki aliarifu kwamba Upyaisho Karismatiki Katoliki sasa umeenea

karibu katika kila nchi duniani.

Kupokelewa na Vatikano

Mwezi Octoba 1973, Papa Paulo VI alifanya mkutano wa pekee na viongozi 13 walioshiriki

mkutano wa kimataifa wa viongozi wa Upyaisho Karismatiki Katoliki mjini Roma. Katika mkutano

huu Papa alisema maneno ya kutia moyo UKK. Katika mikutano na viongozi wa UKK , mapapa

Paulo VI na Yohani Paulo II, wameendelea kutia moyo na kufurahia utendaji wa UKK. Mwanzoni

mwa miaka ya sabini Papa Paulo VI alimuomba Leo Kardinali Suenens achukue jukumu la

kichungaji kwa UKK.

Mwaka 1993, hati maalumu ya kanisa ilitolewa nakatika kutambuliwa huko jina rasmi

likabadilishwa na kuwa ‘Huduma ya Kimataifa ya Upyaisho Karismatiki Katoliki’ (International

Catholic Charismatic Renewal Services – ICCRS).

Upyaisho Karismatiki Katoliki kote duniani hadi Tanzania

Hadi sasa UKKK umepokewa karibu katika nchi zote za dunia. Hapa Tanzania vikundi vya sala

vimeenea katika parokia nyingi kwa idhini ya maparoko na katika majimbo mengi maaskofu

wameonyesha ushirikiano , ukaribisho mkubwa na nia nzuri ya kutaka kusaidia kulea vuguvugu

hili.



Ni vyema ifahamike kuwa ukimya uliotawala katika kufanyia kazi kwa haraka upyaisho wa Roho Mtakatifu ndani ya kanisa ulifanya karismatiki ya kipentekoste kuenea na hivi hata baadaye baadhi ya wakatoliki kama wale walioshiriki wikiend ya Dequene  kuombewa Roho Mtakatifu na madhehebu ya kipentekoste. Huu ni kwa hakika Uekumene wa kiroho kwani tunashirikishwa vipawa vya Mungu kwa namna ambavyo Mungu mwenyewe amekusudia.



Ni vyema Karismatiki Katoliki ikaendelea kujiimarisha zaidi katika kuhubiri injili, kujifunza mafundisho ya kanisa na kuhimiza yale yanayotoka kwa mababa wa kiroho bila kupuuza.

Comments

Popular posts from this blog

IFAHAMU KARISMATIKI KATOLIKI

SEHEMU YA PILI.